KICHWA CHA ALIYEKUWA MWANAFUNZI WA IFM JAMES TEMBA CHAPATIKANA .


 

HABARI Kichwa cha marehemu James Temba, ambaye alizikwa siku chache zilizopita baada ya kuuawa kikatili, kimepatikana katika eneo la Kitunda Kibeberu, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. 


Taarifa hiyo imethibitishwa na baba mzazi wa marehemu, Mzee Temba, ambaye amesema walipokea taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi kuhusu kupatikana kwa sehemu hiyo ya mwili wa mwanawe.


Mzee Temba amesema kuwa baada ya kukamilika kwa taratibu za kiupelelezi zinazofanywa na Jeshi la Polisi, familia itafanya maandalizi ya kuhifadhi kichwa hicho karibu na sehemu ilipozikwa mwili wa marehemu. 


Ameeleza kuwa wakati wa mazishi ya awali ya kiwiliwili cha James Temba, familia iliacha nafasi maalum ya dharura iwapo kichwa kingepatikana ili kiweze kuzikwa kwa heshima stahiki pamoja na mwili wake.


Aidha, Mzee Temba amelishukuru Jeshi la Polisi kwa juhudi za ufuatiliaji zilizosaidia kupatikana kwa kichwa hicho. 


Pia ametoa shukrani kwa ndugu, jamaa, marafiki, Watanzania pamoja na waandishi wa habari kwa kuendelea kuwa pamoja na familia yake katika kipindi chote kigumu cha maomboleza ya kifo cha mwanawe. 



Powered by Blogger.