KISA JUMBA LA MAAJABU YANGA YAKIONA CHA MOTO YAPIGWA FAINI NZITO

 





Yanga SC imetozwa faini ya shilingi milioni 30 (Milioni Thelathini) kwa kosa la wachezaji na maofisa wake wa ufundi kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo na badala yake walitumia nyumba iliyo nje ya uwanja.

.

Klabu ya Yanga pia imepewa Onyo Kali kwa kosa la kuchelewa kuwasili kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Kuelekea mchezo wa Dabi ya Kariakoo ya Mei 3, 2026.

.

Yanga SC iliwasili uwanjani saa 10:35 alasiri badala ya saa 10:30 alasiri jambo ambalo ni kinyume na matakwa ya Kanuni ya 17:15 ya Ligi Kuu ya NBC kuhusu taratibu za mchezo.

.

VIPI ADHABU INATOSHA ?

.

Powered by Blogger.