MAYELE AWAPA KOMBE LA FA PYRAMIDS FC
Fiston Mayele ameendelea kung’ara akiwa na klabu yake ya Pyramids FC, baada ya kufunga goli muhimu katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya ZED FC, matokeo yaliyoiwezesha timu hiyo kufuzu hatua inayofuata ya Kombe la Misri FA Cup.
Mayele aliifungia Pyramids goli la pili dakika ya 57, huku mabao mengine yakifungwa na Karim Hafez dakika ya 44+1 kwa mkwaju wa penalti na Rafaat Khalil akifunga kwa ZED FC dakika ya 90+2.
Nyota huyo ameendelea kuwavutia mashabiki wa soka kwa kiwango chake bora, huku akiisaidia Pyramids kuandika historia na kuendelea kuwa miongoni mwa timu imara zaidi nchini Misri.
FT: ZED FC 1-2 Pyramids
⚽ 90+2’ Rafaat Khalil
⚽ 44+1’ Karim Hafez (P)
⚽ 57’ Fiston Mayele

