RAIS RUTO AWASILI NCHINI

 


Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto



CGH, amewasili nchini Tanzania kwa Ziara ya Kitaifa ya Siku Mbili, Mei 4 na 5, 2026.


Mheshimiwa Ruto atapokelewa kwa gwaride la heshima na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Dar es Salaam ambapo pia watafanya mazungumzo ya uwili ili kuimarisha uhusiano wa Tanzania na Kenya.


Mapema kesho, Mei 5, 2026, Mheshimiwa Ruto atalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma kabla ya kuhitimisha ziara yake.

Powered by Blogger.