MZALENDO ALPHONCE MUYINGA AWAGUSA WAZAZI,WALIMU NA WANAFUNZI DODOMA.

 



Leo tarehe 4/5/2026 katika makao makuu ya nchi, jijini Dodoma, Mzalendo Alphonce Muyinga (Alphanga Black) ameacha alama ya kipekee ya uzalendo na kujitoa kwa jamii baada ya kutembelea Shule ya Msingi Michese.


Akiwa shuleni hapo, amewagusa kwa karibu wazazi, walimu na wanafunzi kwa kuwahamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii, akisisitiza kuwa elimu ndiyo msingi wa mafanikio yao binafsi, familia zao na taifa kwa ujumla.



Katika kuunga mkono jitihada za serikali chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassan, hasa katika kuhakikisha mazingira bora ya kujifunzia na matumizi ya nishati safi na salama, Alphonce Muyinga ametoa msaada mbalimbali ikiwemo:


Vyakula vya lishe kwa ajili ya wanafunzi


Mitungi miwili mikubwa ya gesi pamoja na jiko la kisasa ili kusaidia matumizi ya nishati safi


Daftari 800


Kalamu (box 10)


Sabuni za kunawia mikono (box 3)


Taulo za kike (box 4)


Dawa za kusafishia vyoo (lita 30)


Sukari kilo 50 kwa ajili ya uji wa wanafunzi



Aidha, hakuwasahau walimu ambapo alichangia shilingi laki tano (500,000) katika kikoba cha walimu pamoja na shilingi laki mbili (200,000) kusaidia lishe ya watoto, ikiwa ni sehemu ya kuwapa moyo na kuthamini mchango wao mkubwa katika malezi na elimu.


Akihitimisha, Mzalendo Alphonce Muyinga alitoa wito mzito kwa Watanzania wote akisema:

Kabla ya kujiuliza taifa limetufanyia nini, tujiulize sisi tumelifanyia nini taifa.


Alisisitiza kuwa kila Mtanzania ana wajibu wa kushiriki katika kuimarisha elimu, kuwalea watoto katika maadili mema, na kuwatia moyo walimu ili kujenga taifa imara kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Powered by Blogger.