SIMBA YAIFUATA YANGA KMC COMPLEX
Klabu ya Simba imeutangaza uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, Dar es Salaam kuwa uwanja wao wa nyumbani, wakirejea uwanjani hapo kutoka uwanja Meja Janerali Isamuhyo waliokuwa wakiutumia tangu mwanzo wa msimu.
Itakumbukwa uwanja wa KMC Complex ndio makazi ya mahasimu wao wakubwa, Yanga SC kama uwanja wao wa nyumbani hivyo Mnyama na Wananchi watautumia uwanja huo pamoja mpaka itakavyotangazwa vinginevyo.

