VIJANA ACT WATAKA WIZARA YA VIJANA ITENGE FEDHA NYINGI KWA VIJANA.

 



Na Mwandishi wetu

Dar es salaam

Chama cha ACT wazalendo kupitia mwenyekiti wa ngome ya vijana wa chama hicho Taifa,Abdul Nondo kimeeleza kusikitishwa na kiasi cha shilingi Bilioni 28  ambazo zimetengwa kwa ajili ya Chai na mambo mengineyo huku  Bilioni. 4 Pekee. Zikiwa ni kwa ajili Mikopo kwa Vijana.


 Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya ACT Wazalengo, ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari wakati akichambua bajeti ya Maendeleo ya Vijana, iliyosomwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mheshimiwa Joel Nanauka, Bungeni




Amesema kuwa kuwa vijana wanatakiwa kupatiwa mikopo ambayo imetengwa na wizara hiyo bila kuwa na ubauzi Wala masharti kandamizi.




Nondo ameongeza kuwa kumekuwa na masharti Mengi kwa vijana wanaoomba mikopo hiyo hivyo kuishauri Serikali kutumia namba au vitambulisho vyao vya NIDA Pekee kwenye nyaraka zao badala ya mlolongo mrefu wa nyaraka ambazo nyingine ni ngumu kuzipata.


Hata hivyo ameshauri kuwa wizara ya maendeleo ya vijana inabidi iongeze fedha za mikopo kwa vijana.

Powered by Blogger.