WAZIRI KIJAJI ATOA VIPAUMBELE TISA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA 2026/2027*

 



Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ametaja vipaumbele tisa vya utakelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2026/2027.


Akiwasilisha bajeti ya Wizara yake leo tarehe 15 Mei, 2026 Jijini Dodoma Waziri Kijaji ametaja Vipaumbele hivyo kuwa ni Kuimarisha uhifadhi, ulinzi, na matumizi endelevu ya rasilimali,  Kuimarisha miundombinu utalii, Kutangaza utalii ndani na nje ya nchi na Kuendeleza na kuboresha mazao ya utalii (MICE).


Vipaumbele vingine ni pamoja na Kuimarisha uzalishaji, kuongeza masoko ya mazao ya misitu na nyuki, Matumizi ya teknolojia za kisasa katika usimamizi wa rasilimali na ukusanyaji wa mapato na Kuimarisha Utafiti, Ubunifu na Maendeleo ya Rasilimaliwatu.


Ameongeza kuwa vipaumbele vingine ni 

mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni zinazoendana na mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kiteknolojia pamoja na Kuboresha mazingira ya kazi, mifumo ya usimamizi wa utendaji na uwajibikaji.


Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyowasiliahwa Bungeni jijini Dodoma itajadiliwa kwa siku mbili leo tarehe 15 na 18 Mei, 2026

Powered by Blogger.