MBARONI KWA KUHUJUMU MIUNDO MBINU YA TANESCO

 



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limemkamata na linamhoji Hamis Ajili (20) mkulima, mkazi wa Kata ya Migongo Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za kuharibu na kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).


Kwa mujibu wa taarifa ya leo Juni 01, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP, Issa Suleiman, mtuhumiwa amekamatwa mnamo tarehe 30.05.2026 katika Kijiji cha Mnarani Kata ya Marika akiwa na vipande sita vya nyaya za umeme aina ya Kopa mali ya Shirika la Umeme Tanzania mkoa wa Mtwara.


Taarifa hiyo imesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwabaini washirika wake na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa kwenye mamlaka nyingine za kisheria.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limetoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kujihusisha na uhujumu wa miundombinu ya serikali ambayo imekuwa ikikwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo.



Powered by Blogger.