WATAALAM WA REA ZAMBIA KUJIFUNZA MAFANIKIO YA TANZANIA KATIKA USAMBAZAJI UMEME VIJIJINI*

 



Viongozi wa Mamlaka ya Nishati Vijijini (REA) kutoka nchini Zambia wamewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kujifunza na kubadilishana ujuzi na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).


REA Zambia ambao wameongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Zambia anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Arnold Simwaba wamewasili leo Juni 21, 2026 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Tanzania, Wilson Nyamanga pamoja na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kiutoka REA Tanzania, Mhandisi Jones Olotu, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa REA Tanzania, Renatus Msangira.




Uongozi wa REA Zambia utakuwa nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku 7 ambapo pamoja na vikao vya kubadilishana ujuzi, wajumbe hao wanatarajiwa kutembelea miradi mbalimbali ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini.

Powered by Blogger.