OLIVIA CHAGULA AHIMIZA UPANDAJI MITI.

 



Na Mwandishi Wetu


WATANZANIA, Viongozi, pamoja na Sekta mbalimbali zimeombwa kuhakikisha zinawahimiza kuona umuhimu wa kupanda miti ya vivuli pamoja na miti ya matunda.


Wito huo ulitolewa Jijini Dar es Salaam Jana na mmoja wa viongozi aliyekuwa mgombea  wa ubunge viti maalum Taifa mwaka 2025 kupitia Umoja wa Wazazi Jumuiya ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mfanyabiashara Olivia Chagula.


Hayo aliyasema wakati wa kongamano la upandaji miti  katika maeneo mbalimbali kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Samialism inayojihusisha na masuala mbalimbali ya kitaifa Chini ya Mwenyekiti wake Taifa Charles Sabiniani maalufu kama (Lowassa).


Alisema viongozi wote kwa kushirikiana na Serikali wanatakiwa kuona umuhimu wa kuwaelekeza watoto wao na vijana wote wa kitanzania juu ya umuhimu wa kupanda miti na kuweka mazingira katika hali mzuri.




"Unajua kuna jambo muhimu sana ambalo tunatakiwa kulijua kwamba hii miti inatusaidia katika mambo mbalimbali kupata matunda, vivuli, kuzuia mmomonyoko wa ardhi na mambo mengine mengi hivyo kuna haja ya kuhakikisha jambo hili linapewa uzito zaidi kwa vijana wetu na watanzania kwa ujumla lakini pia kwa kujua kwamba tunamuunga mkono Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan"; alisema Mfanyabiashara huyo Olivia.


Mwenyekiti Lowassa, alisema kuwa zoezi la kupanda miti halitaishia hapo bali Taasisi yake kwa kushirikiana na wadau wengine wataendelea kupanda miti hiyo maeneo mbalimbali lengo likiwa ni kuunga mkono juhusi za Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


Katika kongamano hilo wadau mbalimbali wa mazingira waliudhuria ambapo Mwanadiplomasia na Mratibu wa Makongamano ya Vijana, Omary Abdall Punzi alisema yeye akiwa kiongozi anaamini mkusanyiko wa viongozi mbalimbali waliokusanyika na kujadili masuala ya Kitaifa utaleta tija kwa Taifa.


Punzi ambaye pia ni Mjumbe wa Bosi ya Wakurugenzi Movement for the Federation of East Africa, pia aliwaomba vijana kujiunga na kuwekeza katika Sekta mbalimbali, kuchangamkia fursa pamoja na utumzaji wa Amani pamoja na kuwa na Uadilifu katika Kazi.



Powered by Blogger.