TANESCO LAJA NA MFUMO SMART HOUSE KUFUNGA kWENYE NYUMBA UKIFUATILIA MATUMIZI YA UMEME
Na Mwandishi wetu-Dar es salaam
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limekuja rasmi mfumo mpya wa kufunga nyaya kwenye nyumba smart house. ambao utamwezesha Matumiaji kufuatilia matumizi Vifaa vyake vya Umeme kupitia simu ya mkononi ya Mkononi popote alipo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange amesema Leo Julai 13,Wakati akizungumzia mambo muhimu aliyomueleza Rais Wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi alipotembeleza banda hilo lililopo katika maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba.
Amebainisha kuwa kupitia mfumo huo, simu itakuonyesha chombo gani ndani ya nyumba kinatumia umeme zaidi kwa hiyo unaweza akakizima huko huko uliko Kupitia simu Yake
“Hata kama uko Mwanza, Dubai nyumba iko Dar es salaam au Dodoma unaweza uka switch off hicho kifaa ili matumizi yale unayoyahofia yakasimama,” Twange
amesema Twange na ameongeza kuwa a ubunifu huo umetokana na Shirika kupata malalamiko kadhaa kutoka kwa wateja Kupitia namba 180 kwamba matumizi sio makubwa lakini umeme kuisha haraka.
Hata hivyo amebainisha kuwa malalamiko mengine ni mita kutokusoma vizuri na kuwataka TANESCO imekwenda kufanya ukaguzi hivyo mfumo huo utatoa suluhu ya kujua chombo kinachotumia umeme mwingi ndani ya nyumba.
Amesema hiyo ni teknolojia mpya ambapo wataizindua muda si mrefu kuisambaza kwa wateja jambo linaloonesha kuwa wahandisi wameumiza vichwa na ufumbuzi umepatikana u mezani.
Amewataka wateja wa umeme kuendelea kujua kwamba kila siku wanaumiza vichwa kadri wanavyopata changamoto kutoka kwao na wanaumiza vichwa vya kutafuta suluhu ya changamoto zao.
Hata hivyo alimshukuru sana Rais zanzibar Dkt Mwinyi kupata muda wa kutembelea banda la tanesco na kuona mambo mengi wanayoyfanya.
Amesema amemweleza Rais Dkt Mwinyi hatua zinazochukuliwa na Shirika juu ya kutekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia na kwamba wameshapewa maelekezo ambapo wanatengeneza mbinu tofauti tofauti za kutekeleza
” kwa hiyo kwa sasa tuna mpango unaitwa ni bill financing ambao
unaendelea hapo wateja wetu ambao ni wapya na wale ambao tayari wanatumia umeme wanaweza wakakopeshwa majiko na wakawa wanalipa mkopo wao kadri wanavyonunua umeme,” amesema.
.
Amesema mpango umekuwa na mwitikio mzuri wa mafanikio zaidi ya asilimia 90 kwa hiyo umefanikiwa na ndio maana wameingia kwa sekta binafsi ambao wako nao kama wadau.
“Tumesaini nao mikataba na tumeanza kazi ya kukopesha majiko haya kwa wananchi kwa hiyo naendelea kutoa wito kwa wananchi wote wasiogope kutumia umeme tayari wenzao wameshaonyesha njia hii ndio nishati nafuu zaidi kuliko nishati zingine,” amesema na kuongeza kuwa wanasayansi na wahandisi wameshatengeneza majiko ambayo yanatumia umeme rafiki na utafurahi ukilinganisha na gharama unazitumia kutumia nishati nishati nyingine.
Aidha amesema amemueleza Rais Dkt Mwinyi kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa kujenga njia mpya za kusafirisha umeme kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar.
Amesema katika mradi huo utakuwa na njia za umeme tatu za kupita chini ya maji ikiwa inatoka Dar es Salaam kwenda Unguja kutoka Tanga kwenda Pemba na ya kwenda Mafia.
Amesema ule ni mradi mhandisi mshauri atapatikana Agosti na wanatarajia kumpata mkandarasi Januari na muda wa utekelezaji ni miezi 20, 22.
Twamge amesema mradi kukamilika kwake utaongeza uwezo wa kupeleka umeme mwingi zaidi zanzibar ambayo imejengwa sana katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Dkt Mwinyi.

