MAMIA WAFURIKA KUSHUHUDIA UZINDUZI WA KIHISTORIA WA JNHPP

 




MAMIA  ya wananchi, viongozi na wadau mbalimbali wamefika katika eneo la Rufiji, Mkoa wa Pwani, kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) leo, Agosti 22, 2026.


Uzinduzi huo unaofanyika katika eneo la mradi umevuta umati mkubwa wa watu, huku Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.




JNHPP, wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115, ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati katika sekta ya nishati nchini, ikiwa na lengo la kuongeza uzalishaji wa umeme na kuimarisha upatikanaji wa nishati ya uhakika.




Hafla hiyo imewakutanisha viongozi wa Serikali, wananchi, wadau wa sekta ya nishati na wageni mbalimbali wanaoshuhudia hatua hiyo muhimu katika historia ya maendeleo ya nishati nchini.




Uzinduzi wa JNHPP unatarajiwa kuashiria hatua mpya katika juhudi za Tanzania kuongeza uwezo wa kuzalisha umeme, kupunguza changamoto za upatikanaji wa nishati na kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za kiuchumi na uzalishaji.

Powered by Blogger.