MFUKO WA MF WAENDELEA KUPANUA HUDUMA ZA MIKOPO KWA WANANCHI

 









Mwandishi Wetu,- Dar es Salaam


MFUKO wa Self Microfinance Fund(MF) katika Utendaji wake umeendelea kupanua wigo wa huduma za mikopo nafuu kwa wananchi, hususan wakulima, wafugaji na wajasiriamali,na wafanyabiashara ili kuwawezesha kukuza shughuli zao za kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa.


Hatua hiyo ni moja kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa mfuko huo, ikiwamo kuwapa wananchi fursa ya kupata huduma za kifedha za mikopo na kuondoa dhana kwamba Watanzania hawakopesheki kutokana na changamoto za urejeshaji wa mikopo katika taasisi za kifedha.


Ameyasema hayo Oktoba 28,2026 Ofisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo, Santiel Yona, wakati wa kikao kazi kati ya taasisi hiyo, Ofisi ya Msajili wa Hazina pamoja na wahariri wa vyombo vya habari, jijini Dar es Salaam, kilicholenga kueleza mafanikio yaliyopatikana na Utendaji wake katika kuwakwamua wananchi kiuchumi




Santieli amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025, mfuko huo umechangia upatikanaji wa ajira 262,624, huku ukiendelea kutoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali.


Sambamba na hayo amesema mfuko huo una uwezo wa kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 54, hivyo Watanzania wanatakiwa kutumia fursa hiyo kuendeleza shughuli zao za uzalishaji na biashara.


Akizungumzia urejeshaji wa mikopo, amesema kiwango cha urejeshaji kimefikia asilimia 95, hali inayoonesha mwenendo mzuri katika usimamizi wa mikopo inayotolewa na taasisi hiyo.


"Katika utoaji mikopo kwa Wakulima tumekuwa wanapochelewesha kurejesha hatutumii Sheria kwani tunatambua wakati mingine wanakwama kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hivyo wanakuwa hawajavuna viziri hivyo tunapotathimini na kujiridhisha tunawasongezea siku za kurejesha mikopo badala ya kuwataifisha na wamekuwa wakirudisha "amesema Ofisa Santieli


Hata hivyo amsema mfuko umeweka mikakati ya kuendelea kuimarisha urejeshaji wa mikopo kwa kufanya tathmini ya uwezo wa wakopaji, kuchunguza sababu zinazowafanya baadhi yao kushindwa kulipa kwa wakati na kuweka utaratibu wa kuwasaidia kurejesha mikopo yao.


Pia amefafanua kuwa hatua hizo ni pamoja na kuingia mikataba mipya pale inapohitajika na kuwaongezea wakopaji muda wa kurejesha mikopo kulingana na taratibu zilizowekwa.


“Aliyekopa ni lazima arejeshe fedha alizokopa. Tunaweza kumuongezea muda wa kulipa hadi miaka miwili, kuingia naye mkataba mpya na kujua sababu zilizomfanya ashindwe kurejesha mkopo wake kwa wakati,” amesema Santieli


Kwa upande wake, Manongi mesema katika kipindi cha miaka mitatu, Self Microfinance Fund imefanikiwa kufungua matawi 12 yanayotoa huduma katika kanda mbalimbali nchini, hatua inayolenga kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi.


Pia mafanikio mengine ni pamoja na kutoa gawio la Sh milioni 490.9 na kupata faida ya Sh bilioni 3.19 baada ya kodi.


Hata hivyo , mesema mfuko huo unashiriki katika juhudi za kukuza matumizi ya nishati safi kupitia mradi wa mikopo ya majiko yanayotumia umeme kwa ufanisi, kwa kushirikiana na kampuni ya Positive Cooker.


Sanjari na hayo ameongeza kuwa mfuko huo pia unatoa mikopo kwa ajili ya ununuzi wa bajaji na pikipiki, zinazoweza kutumiwa na wajasiriamali wadogo katika kuendesha na kupanua shughuli zao za kiuchumi.

Powered by Blogger.