EASTER AOMBA MSAADA KWA WATANZANIA
Na Mwandishi wetu, MOROGORO
Mtoto Esther Daudi Athanas (9) mkazi wa Kijiji cha Ruhembe, Tarafa ya Mikumi Mkoani Morogoro, amelazimika kukaa nyumbani kwa muda wote kutokana na kukosa msaada wa matibabu ya changamoto kutoa haja kubwa kupitia tumboni.
Mkaguzi Shayo amesema, Siku ya Mei 20, 2024 Easter akiwa anacheza na watoto wenzake mtaani alimuona Askari Polisi Shayo Ambaye ni Polisi Kata wa Kata ya Ruhembe ghafla akakimbia nyumbani kumwambia dada yake kuwa anataka amfuate yule Askari ili amuombe msaada wa kupata matibabu ili na yeye aweze kwenda Shule kama wenzake kwa kuwa anatamani s ana kusoma kama ndugu zake. Alimfuata Polisi Kata na kuanza kumlilia machozi ili amsaidie apate matibabu ya tatizo alilonalo na baadae aweze kwenda Shule .
Kiu ya Easter ni kutibiwa na kwenda Shule.
Polisi Kata wa Shayo ameendelea kusema kuwa Esther wamezaliwa mapacha ambaye pacha mwenzake anasoma darasa la pili katika shule ya Msingi Kitete iliyopo Katani hapo.
“Katika familia yao nzima wapo watoto 6 ambapo wengine ni wakubwa zake, pacha wake Easter yupo darasa la pili shule ya msingi Kitete,”amesema Shayo
Mkaguzi Shayo ameendelea kusema kuwa Easter amezaliwa na tatizo la kupata haja kubwa kupitia ubavuni(tumboni) na si kwa njia ya kawaida.
“Tatizo hilo limesababisha yeye kushindwa kusoma shule kama pacha wake kwa kuwa amekuwa wa kufungwa vibwende na mama yake ili haja kubwa inapotoka izuiwe na vibwende hivyo,”amesema.
Amesema Mama yake Easter ni bubu ambaye hawezi kuzungumza ambapo baba yake aliondoka nyumban miaka mitatu iliyopita na kuwaacha wao na mama yao pekee.
“Mama yake Esther hana kazi yoyote zaidi ya kulima vibarua kwenye mashamba ya watu ili kupata chakula cha kujikimu yeye na watoto wake,”amesema.
Mawasiliano ya Mkaguzi Shayo -0675 325 388