SERIKALI YATOA MIL. 800 KUREJESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA - MALINYI



Na Mwandishi wetu, MOROGORO 

SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan  imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 800 kwa ajili ya ukarabati wa barabara za Igawa - Malinyi, Lugala - Misegese, Njiapanda - Malinyi zilizoatbiriwa na kusambaa kwa mto furua na kuharibu barabara inayohudumiwa na TANROADS pamoja na zile zinazohudumiwa na TARURA.

Kutokana na changamoto hiyo wananchi wa Malinyi hawana mawasiliano kwa kuwa barabara zinazounganisha wilaya hiyo pamoja na ile ya kuelekea Ifakara zimeharibika vibaya na kusabisha adha kubwa kwa wananchi hao.

Ni siku ya pili ya ziara ya Waziri Mchengerwa akiwa mkoani Morogoro ambapo Mei 21, 2024 yupo Wilayani Malinyi na kukagua miundombinu ya barabara za Mji wa Malinyi na kujiridhisha kuwa miundombinu hiyo imeharibiwa vibaya na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni na kwa niaba ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Waziri Mchengerwa amesema fedha za dharura zipelekwe haraka kurejesha mawasiliano ya barabara ya Kichangani.


Hata hivyo, amuagiza Meneja wa Wakala ya ,Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Morogoro Eng. Emmanuel Ndyamukama kutangaza zabuni hiyo ndani ya wiki na mkandarasi atakayepatikana aanze kujenga barabara hiyo haraka huku mawasiliano yakiendelea kufanyika na Wizara ya Ujenzi ili kuona namna ya kujenga Daraja la Mto Furua lilichukuliwa na maji na kukata mawasiliano ya barabara hiyo.

‘nimeshawaelekeza watendaji wa Wizara yangu Naibu Katibu Mkuu anayesimamia miundombinu ambaye ndiye anayewasimia  TARURA kuleta fedha hizo kwa Meneja wa TARURA mkoa amesema wanahitaji Mil. 800, nimewapa wiki mbili nataka Barabara hii ipitike…’’Amesema Waziri Mchengerwa.

Sambamba na hilo, Mohamed amewataka viongozi wa ngazi zote kushirikiana  na kuwa wabunifu ili kuwatumikia wananchi kikamilifu huku akiwaagiza Wakuu wa Mikoa yote Tanzania Bara kuitisha vikao vya dharura na wataalamu wote ndani ya Mikoa yao pamoja na wadau wa Maendeleo ili kujadili na kurejesha mawasiliano ya Barabara zilizoharibiwa na mafuriko.


Powered by Blogger.