FAINALI CRDB , YANGA VS AZAM KUKIPIGA Z'BAR

 Fainali ya Kombe la Shirikisho la benki ya CRDB iliyokuwa ifanyike Juni 2 Babati Mkoani Manyara, sasa itafanyika Zanzibar katika uwanja wa New Amaan.

Taarifa iliyotolewa na TFF inaeleza kuwa baada ukaguzi wa uwanja wa Babati, imebainika baadhi ya miundombinu haiko vizuri kuwezesha mechi kuchezwa hapo, ikiwemo pia suala la usalama.

Mechi hiyo itaikutanisha miamba ya soka nchini, Mabingwa mara 30 wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young African SC dhidi ya 'Matajiri' wa Chamazi Azam FC


Powered by Blogger.