𝗠𝗪𝗘𝗡𝗬𝗘𝗞𝗜𝗧𝗜 𝗞𝗔𝗪𝗔𝗜𝗗𝗔: 𝗡𝗜𝗠𝗣𝗢𝗡𝗚𝗘𝗭𝗘 𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗞𝗨𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗔 𝗞𝗨𝗟𝗘𝗧𝗔 𝗠𝗔𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗢
Na Mwandishi wetu,DODOMA
Mwenyekiti wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mohammed Ali Kawaida amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuleta maendeleo hususani ahadi alizotoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu katika siku 100 za kwanza za uongozi wake.
Kawaida akizungumza na maelfu ya wanafunzi wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu mkoani Dodoma leo tarehe 24 Januari 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.
Ametaja baadhi ya yaliyotekelezwa ikiwemo Bima ya Afya kwa wote na ajira kwa vijana zikiwemo za udaktari.




