SIMBA YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR NYUMBANI
Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Wekundu wa msimbazi Simba sports Club leo hii imeambulia sare yakufungana goli moja kwa moja dhidi ya timu ngumu ya Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro.
Simba ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Meja Isamuyo mbele ya mashabiki wake walifanikiwa kupata goli mnamo dakika ya 19 kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Eliu Mpanzu na kwenda mapunziko wakiwa kifua mbele.
baada ya kipindi cha pili kuanza timu ya mtibwa ilionekana ikicheza kwa nidhamu kubwa kwa kuwaheshimu Simba ambapo mnamo dakika ya 60 ya mchezo Mgata Charles alisawazisha kwa shuti kali la nje ya kumi na nane nakumuacha goli kipa wa Wekundu wa msimbazi asiwe na cha kujitetea .
Mpaka dakika tisini SIMBA 1 - MTIBWA 1

