𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔 𝗔𝗠𝗘𝗪𝗘𝗞𝗔 𝗝𝗜𝗪𝗘 𝗟𝗔 𝗠𝗦𝗜𝗡𝗚𝗜 𝗠𝗥𝗔𝗗𝗜 𝗪𝗔 𝗨𝗝𝗘𝗡𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗔𝗡𝗞𝗜 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗣𝗢𝗞𝗘𝗔 𝗠𝗔𝗙𝗨𝗧𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗕𝗔𝗡𝗗𝗔𝗥𝗜 𝗬𝗔 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠

 


𝙈𝙧𝙖𝙙𝙞 𝙝𝙪𝙪 𝙪𝙣𝙖𝙩𝙚𝙠𝙚𝙡𝙚𝙯𝙬𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙛𝙚𝙙𝙝𝙖 𝙯𝙖 𝙣𝙙𝙖𝙣𝙞 𝙯𝙖𝙞𝙙𝙞 𝙮𝙖 𝙏𝙨𝙝 𝘽𝙞𝙡𝙞𝙤𝙣𝙞 678

𝙐𝙢𝙚𝙡𝙚𝙩𝙖 𝘼𝙟𝙞𝙧𝙖 𝙯𝙖 𝙢𝙤𝙟𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙤𝙟𝙖 𝙯𝙖 𝙢𝙪𝙙𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙒𝙖𝙩𝙖𝙣𝙯𝙖𝙣𝙞𝙖.

𝙆𝙪𝙨𝙖𝙞𝙙𝙞𝙖 𝙠𝙪𝙥𝙪𝙣𝙜𝙪𝙯𝙖 𝙪𝙝𝙖𝙗𝙖 𝙬𝙖 𝙢𝙖𝙛𝙪𝙩𝙖 𝙣𝙘𝙝𝙞𝙣𝙞 𝙣𝙖 𝙢𝙪𝙙𝙖 𝙬𝙖 𝙢𝙚𝙡𝙞 𝙠𝙪𝙨𝙪𝙗𝙞𝙧𝙞.

𝙆𝙪𝙤𝙣𝙜𝙚𝙯𝙖 𝙢𝙖𝙥𝙖𝙩𝙤 𝙮𝙖 𝙏𝙖𝙞𝙛𝙖.

Na Mwandishi wetu,DAR 

Rais Tanzania  Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 ameweka jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Matanki ya kupokea Mafuta katika Bandarinya Dar es salaam upande wa Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam, leo tarehe 03 Machi 2026.

Ujenzi wa Matanki hayo utasaidia kupunguza na kuondoa kabisa uhaba wa mafuta Nchini, kuimarisha usalama wa nishati hiyo, kupunguza muda wa meli kusubiri nangani kutoka wastani wa siku 22 hadi siku 7, kupunguza muda wa kushusha shehena ya mafuta kutoka siku 7 hadi siku 1.

Vilevile, utasaidia kuongeza mapato ya Taifa kupitia makusanyo ya kodi na tozo mbalimbali zitakazo kusanywa na Mamlaka husika pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania.






Powered by Blogger.