MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI APEWA MAAGIZO NA BUNGE,SERIKALI
SPIKA wa Bunge Mussa Zungu amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Hamza Johari kuchukua hatua kali dhidi ya Taasisi na Mashirika ambayo yalikaidi ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Utekelezaji wa Mikataba ya miradi mbalimbali kama ilivyoripotiwa na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG
Ameyasema hayo jana Aprili 1,2026 Bungeni Dodoma wakati wa hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2026/27
Wakati huo huo Nae Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba amemuelekeza Mwanasheria huyo Mkuu kukaa pamoja na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI ili waandae mpango mkakati madhubuti katika kuhakikisha kwamba wanapata ufumbuzi wa kudumu juu ya migogoro ya ardhi inayoongezeka kila siku na kuwa kero kwa Wananchi.

