WAZIRI KAPINGA AKAGUA MAENDELEO YA MAANDALIZI MAONESHO YA 50 YA BIASHARA (SABASABA)
Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya maandalizi ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, mkoani Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Waziri Kapinga ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania TANTRADE kwa maandalizi mazuri yaliyofanyika hadi sasa.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi ili kuhakikisha maonesho hayo yanafanyika kwa mafanikio makubwa, hususan katika mwaka huu ambao yanaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Dkt. Latifa Mohamed Hamis, amemshukuru Waziri kwa kutembelea na kukagua maandalizi hayo.
Aidha amewasilisha taarifa kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa, ikiwemo uhamasishaji wa washiriki, usimamizi wa ukarabati wa mabanda ya maonesho na maboresho ya mifumo ya huduma kwa washiriki na wageni.
Pia alieleza kuwa mwaka huu TanTrade imejipanga kutumia mfumo wa tiketi za kielektroniki ili kurahisisha uingiaji wa wananchi na wageni katika maonesho hayo, sambamba na kuongeza ufanisi na usalama wa huduma zinazotolewa.


