TIRDO YAIBUA WABUNIFU WA AFRO HEAL, WACHAKATA MIMEA YA ASILI KUWA DAWA ZA KISASA

 




Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) limeendelea kuwa chachu ya ubunifu kwa kuiwezesha Afro Heal Group Limited kubadilisha mimea ya asili kuwa dawa za kisasa zenye ubora na viwango vinavyokidhi mahitaji ya soko.




Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane, mwakilishi wa kampuni hiyo, Mashauri Shushu, amesema kabla ya kushirikiana na TIRDO walikuwa wakitengeneza dawa kwa njia za jadi, lakini kupitia malezi ya biashara, ushauri wa kitaalamu na teknolojia waliyoipata, sasa wanazalisha dawa za kisasa zinazorahisisha matumizi na kuchangia kuboresha huduma za afya.


Kishushu amesema TIRDO imekuwa mshirika muhimu katika kuwainua wabunifu wa Kitanzania kwa kuwapa mazingira rafiki ya kukuza mawazo yao na kuyageuza kuwa bidhaa zenye thamani ya kibiashara. 




Pia amewahimiza vijana kuamini katika ubunifu wao, kuwa wavumilivu na kutumia fursa zinazotolewa na taasisi mbalimbali ili kufikia mafanikio.


Afro Heal Group Limited inalenga kupanua uzalishaji wa dawa zinazotokana na mimea ya asili na kuzifikisha katika masoko ya ndani na kimataifa.

Powered by Blogger.