KISWILI AIBUKA MSHINDI BAADA YA KURA KUFUNGANA KATIKA UCHAGUZI WA CCM MAGOMENI

 



Na Mwandishi wetu


UCHAGUZI mdogo wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Magomeni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umemalizika salama  baada ya wagombea watatu kuchuana akiwemo Timo Mmanda, Comrade DR. Jackson Makumbi na Ally Kiswili.


Uchaguzi huo ulifanyika Jijini Dar es Salaam jana katika Kata hiyo ambapo wagombea hao watatu kura zilizopigwa zilikuwa kama ifuatavyo ambapo kura zilizopigwa awali mgombea Timo Mmanda alipata kura 0 wakati wagombea wawili Comrade DR. Jackson Makumbi na Ally  Kiswili walifungamana kwa wote kupata kura 16 kwani wapiga kura walikuwa 32.




Baada ya sintofahamu hiyo Uchaguzi huo uliludiwa kwa wagombea wawili yaani Makumbi na Kiswili ambapo  kura zilipigwa tena na ndipo Kiswili aliibuka mshindi kwa kupata kura 17 na Makumbi... kupata kura 15 hivyo kufanya kura zote zilizopigwa kuwa 32 bila kura yoyote kuharibika.


Uchaguzi ulimalizika na mshindi kutangazwa majira ya saa 11:46 asubuhi.


Mshindi wa nafasi ya pili Makumbi akizungumza baada ya matokeo hayo alisema kuwa anatoa pongezi za dhati kwa wapiga kura na kusema kuwa amekubaliana na matokeo na kwamba atamuunga mkono Mwenyekiti mteule ili Jumuiya ya Wazazi isonge mbele.


Alisema kuwa uchaguzi ni uchaguzi na lazima uheshimiwe na kwamba kishindwa kwake bado kunampa nafasi ya kuendelea kujipanga zaidi katika kuhakikisha anakitumikia Chama.


"Mwenzangu amepata kura 17 na mimi 15, ni dhahili kwamba wapiga kura walikuwa wamejipanga vizuri kumchagua mmoja wapo kati yetu hivyo matokeo yaliyotangazwa yako sahihi na sasa tunaelekea kwenye utekelezaji katika kumuunga mkono Mwenyekiti," alisema Makumbi, na kuongeza;


"Lakini pia nipende kusema kuwa uchaguzi umeisha na Kila kitu kimekwisha hivyo hatuangalii alichoshinda bali dhamana ya Chama aliyobeba kwani chama ndicho kikubwa," alisema.


Aidha, alisema anatoa pongezi kubwa kwa wapiga kura kwani pamoja na kampeini za muda mfupi kutokana na kwamba uchaguzi ni wa mpito  lakini wapiga kura walimuhamini na kumpa kura nyingi ambazo pia zilimfanya kuwa na faraja na kusema kuwa kura alizopata anawashukuru sana wapiga kura.


Mwenyekiti mteule Kiswili, alisema kuwa anawapongeza wapiga kura na kusema kuwa ametoa fursa kuwa atawalipia ada ya uanachama ya miaka miwili Kila mwanachama wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Magomeni lengo kubwa likiwa ni kuwafanya wawe na molali katika utendaji kazi.


Lakini pia alisema zipo changamoto mbalimbali ambazo amepanga kuzishughulikia kubwa ikiwa ni ile ya suala zima la usafi yaani mazingira kwenye hili ninaahidi kufanya jambo kubwa ndani ya Kata ya Magomeni na kuwataka wanachama kwa sasa kuvunja makundi na kuwa kitu kimoja.


"Kwa hiyo hizi ni baadhi ya ahadi zangu ambazo napanga kuzivalia njuga kwa kuzishughulikia huku nikishirikiana na wananchi wangu, lakini kuhusu suala la uchaguzi Kuna kushinda na kishindwa na pia unapokuwa umeingia kwenye kinyanganyiro tunatakiwa kujiamini kwa asilimia zote," alisema Mwenyekiti Mpya.


Msimamizi Mkuu Msaidizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wazazi Wilaya ya Kinondoni Salum Lyeme, alisema kuwa uchaguzi ulienda vizuri ila ulikuwa wa moto sana.


"Pamoja na kwamba wagombea walifungamana lakini hakukuwa na shida yoyote wala kura yoyote iliyoharibika hivyo basi wito wangu kama msimamizi tunaomba wanachama watoe ushirikiano kwa Mwenyekiti mteule ili aweze kutekeleza majukumu yake.



Powered by Blogger.